Goli la dakika za lala salama la kiungo Jonas Mkude katika mchezo wa NBCPL kati ya Tanzania Prisons na Simba Sports Club limetosha kuipa ushindi timu yake ya Simba na kujikusanyia alama tatu muhimu.
KLABU ya Simba Imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya Tanzania prisons kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku wakiendelea na kasi ya kutofungwa msimu huu.
Bao la dakika ya 88 lililofungwa na Jonas Mkude lilitosha kuwapa Simba pointi tatu muhimu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kwa mantiki hiyo hiyo, matokeo hayo ni mapokezi yanayostahili kwa Kocha Mkuu mteule wa timu hiyo JUMA MGUNDA ambaye alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Africa.
Kwa Tanzania Prisons, kipigo hicho kinakuwa cha pili kwenye Ligi Kuu ya NBCPL huku kichapo cha kwanza kikiwa ni kufungwa goli 1-0 na Singida Big Stars.
Katika mchezo wa leo, licha ya kushindwa, walifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo hazikuweza kuzaa matunda hadi kipenga cha mwisho kilipolia.
Septemba 28, Mbeya City watakuwa wenyeji wa Simba huku Azam wakicheza na Tanzania Prisons Septemba 30, michezo yote miwili ikipigwa kwenye Uwanja wa Sokoine.
HILI HAPA GOLI LA SIMBA SC DHIDI YA TANZANIA PRISONS
0 Comments