Ticker

6/recent/ticker-posts

Aziz Ki aleta vita mpya Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


YANGA imeanza Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania, lakini staa mmoja ameibua vita mpya iliyowahusisha viungo sita wa timu hiyo akiwamo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Gael Bigirimana.

Dakika 45 tu zilitosha Yanga kugundua wapi kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz Ki anatakiwa acheze ili kuleta mafanikio ya timu hiyo katika mechi za mashindano.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alimuanzisha Aziz Ki kama winga katika mchezo dhidi ya Simba katika dakika 45 za kwanza, lakini kile cha pili alimrudisha kucheza kama namba 10 nyuma kidogo ya mshambuliaji wa mwisho na jamaa akaonyesha makali katika eneo hilo.

Akihojiwa Nabi alisema alijaribu kumpeleka pembeni Aziz Ki, lakini ilishindikana na sasa anataka kuendelea kumuamini staa huyo wa zamani wa ASEC Mimosas kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho baada ya kuanza kuonyesha makali.

Kwenye mechi mbili alizocheza Aziz KI amezalisha pasi za mabao sita, huku moja ikizalisha bao.

Nabi alisema hatua ya kuendelea kumtumia Azizi KI katika nafasi hiyo italeta vita ya viungo wengine wa kati kuendelea kupigania nafasi mbili pekee za kiungo mkabaji na kiungo mchezeshaji wa juu.

Viungo hao wa kati ni Khalid Aucho, Yannick Bangala, Feisal Salum, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

“Nilitamani angeweza kucheza pembeni ili tutengeneze nafasi pana ya wengine kuweza kupata nafasi ya kucheza, lakini tunaona jinsi alivyo na ufanisi akicheza pale nyuma ya mshambuliaji wa mwisho,” alisema Nabi.

“Tuna viungo sita ambao sasa tutalazimika kuwatumia katika maeneo ya kati pekee. Hili litaleta ushindani zaidi baina yao kuhakikisha wanakuwa katika ubora kuwania nafasi.

“Haitakuwa kazi rahisi kwetu kama makocha katika kuchagua nani anatakiwa kuanza viungo wetu wengi bora ambao kila mmoja anatamani kucheza, tutalazimika pia kuwa na mzunguko wa kuwapa nafasi.”

Yanga imeendelea na rekodi ya kutopoteza mchezo katika Ligi Kuu Bara - ikifikia mechi 38 bila kupoteza katika mashindano hayo.

Post a Comment

0 Comments