Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester United kulipa £60m kwajili ya uhamisho wa Casemiro kutoka Real Madrid

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapaManchester United imewasilisha pendekezo rasmi kwa Real madrid kuhusu nia yao ya kumsajili Casemiro huku wakitaka kufunga dili hilo siku ya Ijumaa, mazungumzo yako kwenye hatua ya mwisho.

Man United imewasilisha pendekezo la ada ya €60m pamoja na nyongeza za €10m huku Real Madrid wakitarajiwa kukubali kiasi hicho ili kukamilisha dili hilo mapema.

Manchester United imempa Casemiro mkataba wa muda mrefu utakaotumika hadi Juni 2026 pamoja na chaguo la msimu zaidi, na anatarajiwa kukubali.

Itachukua takriban saa 48 kukamilisha vipimo vya afya na kisha kuandaa hati na Real Madrid ili kuitia saini, haraka iwezekanavyo.

Post a Comment

0 Comments