Ticker

6/recent/ticker-posts

Mayele: Huu ni Mwaka wa furaha Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa mambo mazuri yanakuja na wameanza msimu huu wa 2022/23 pale walipoishia msimu uliopita.

Nyota huyo ameanza msimu kwa kufunga akiifungia timu yake bao la kwanza katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakati wakishinda mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Wakati akihojiwa Mayele alisema wamerejea katika ligi msimu huu kuendelea walipoishia msimu uliopita kwa sababu wanahitaji kutetea mataji yao yote baada ya kufanikiwa kutwaa Ngao wa Jamii.

Alisema walianza dhidi ya Simba kwa kutetea taji la Ngao ya Jamii, wakafuata Polisi Tanzania kwenye Ligi Kuu kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini jambo ambalo ni mwanzo mzuri kwao.

"Pointi tatu ugenini ni jambo zuri na nimeendelea kufunga, bao la kwanza sasa tunaendelea tulipoishia na tunawahakikishia mashabiki mambo mazuri yanakuja zaidi ya waliyopata msimu uliopita," alisema Mayele.

Alisema kocha Nabi (Nasreddine) ameona mapungufu yao na kuyafanyia kazi ili kutorudia katika mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kesho, Jumamosi.

Post a Comment

0 Comments