Ticker

6/recent/ticker-posts

Yannick Bangala Asalia Yanga hadi 2024

 Yannick Bangala Asalia Yanga hadi 2024

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya soka ya Yanga, imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja Kiungo Mkabaji Raia wa Congo, Yannick Bangala ambapo ataendelee kusalia ndani ya kikosi hicho hadi 2024.

Mchezaji huyo ameongeza mkataba leo mara sambamba na beki Djuma Shabani baada ya kurejea ndani ya kikosi hicho wakitokea mapumzikoni kwao nchini Congo.

Mkaba wa awali wa Bangala ulikuwa unamalizika msimu ujoa ambao unatarajia kuanza hivi karibuni, kufuatia kusaini miaka miwili hapo awali.

Tangu alipo sajiliwa 2021, akitokea klabu ya FAR Rabat ya Morocco, Yannick Bangala amekuwa na msimu mzuri akiwa Yanga.

Pia alifanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha msimu, katika tuzo zilizotolewa na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) tarehe 7 julai 2022 na kushinda tuzo ya Kiungo Bora na Mchezaji Bora.
Post a Comment

0 Comments