Ticker

6/recent/ticker-posts

Karim Mandonga Afunguka Siri Ya Kichapo Kwenye Technical Knock Out

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Karim Mandonga Afunguka Siri Ya Kichapo Kwenye Technical Knock Out
Baada ya kuchapwa kwa Technical Knock Out, Karim Mandonga ametoboa siri ya kipigo huku akiwaomba mashabiki wake kutorudi nyuma.

JE, UNAHITAJI ARIJA? BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI

"Mpinzani wangu alinipiga right (ngumi ya kulia) akaunganisha na left hook, nikayumba, wakati natambalia mikono nikitaka  kunyanyuka refarii akamaliza pambano," amesema Mandonga.


Amesema Mandonga mtu kazi yuko fiti na mashabiki wake wasirudi nyuma kwani kukosea leo sio kukosea kesho.


"Michezo yetu ni ya makosa, ukifanya kosa moja mwenzako tumia kukumaliza, ndicho kimetokea kwangu," amesema.


Mandonga amechapwa kwa TKO na Shaban Kaoneka raundi ya nne ya pambano lililopigwa mjini Songea usiku wa kuamkia leo.


"Nilijitahidi sana kupambana, lakini jitihada zangu ziliishia pale, lakini matokeo yale hayatanirudisha nyuma, sasa nataka kuzichapa na watu wenye rekodi bora kwenye ngumi, hasa wakongwe.


"Nikirudi Dar es Salaam naenda kupiga kambi na mabondia wa Ngome nikajifue jeshini hivyo atajayefuata kazi anayo," amesema.


Kuhusu tambo zake zilizomtambulisha zaidi kwenye ndondi,  Mandonga amesema kila mmoja Mungu kamuandaa na kumpa kipaji chake.


"Naamini mimi kaniandaa hivi na  nafsi yangu ilishakubali kupambana ," amesema bondia huyo anayepigania uzani wa super middle.

Post a Comment

0 Comments