Ticker

6/recent/ticker-posts

simba wazindua rasmi wiki yao majibu ya jezi yapatikana

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KLABU  Simba leo tarehe 31 Julai 2022, imezindua rasmi wiki yao kuelekea kwenye tamasha kubwa la Siku ya Simba (Simba Day), ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali. 

Uzinduzi huo umefanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem, na kuhudhuriwa na viongozi sambamba na wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

Katika uzinduzi uliambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Zuhura Othuman, maarufu kama Zuchu kutoka Wasafi.

Tamasha hili linakuwa kama mlango kuelekea msimu ujao wa mashindano, na mara nyingi hutumika kama sehemu ya kutambulisha kikosi sambamba na benchi la ufundi mbele ya mashabiki.

Akielezea mipango yao kuelekea msimu ujao Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa, klabu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano 2022/23, itakwenda kurejesha makali yake yaliyopotea kwenye msimu uliomalizika huku wakija na kauli mbiu ya kwamba hawazuiliki.


“Nimetoka kule Misri na kitu muhimu ilikuwa kujipanga kwa ajili ya msimu unaokuja, malengo ya klabu yapo palapale tunarudi kwa nguvu tunarudi kurudisha ubingwa wetu, na kauli mbiu yetu kwa msimu huu itakuwa, hatuzuiliki wala hatushikiki,” amesema Barbara.

Kwenye msimu uliomalizika ambao kikosi hicho kilikuwa chini ya kocha Pablo Franco Martin ambaye alifungashiwa virago ndani ya klabu hiyo, hawakufanikiwa kuchukua taji lolote na kuwa na msimu mbaya katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Vituo vya kununua tiketi za Simba Day 2022

Pia uongozi huo uliweka wazi viingilio kwa siku ya tamasha hilo litakalofanyika tarehe 8 Agosti, 2022, ambapo kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 5000, huku kiingilio cha juu kikiwa ni Sh. 30,000.

Tamasha hilo litafanyika jijini Dar es Salaam, kwenye dimba la Benjamin Mkapa kuanzia asubuhi.

Matukio ya wiki hii yataenda sambamba na uzinduzi wa jezi mpya zitakazotumika kwa msimu ujao, ambapo Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa jezi za Simba kwa msimu huu zitatoka Ulaya na sio tena nchini nchina.

“Kuhusu jezi msimu huu tumeacha kwenda kule hung haa (China), safari hii tumekwenda Ulaya, jezi zetu za safari hii zitakuwa zimetoka Ulaya na sio tena Asia na wiki hii tutazindua na tutakuwa vizuri,” amesema Mangungu.

Wakati hayo yote yanafanyika bado uongozi wa klabu hiyo haujaweka wazi, watakwenda kucheza na timu gani kwenye siku hiyo kama sehemu ya mchezo wa kirafiki."Kesho mtajua tofauti ya mdhamini na msaada. Tutakuwa na tukio na mdhamini wetu mpya, kampuni ya M-Bet."

"Wachezaji ambao tunawasajili sio wa sandakalawe, ni wachezaji muhimu kwenye vikosi vyao hivyo kunakuwa na ugumu kuwapata, inabidi kuzungumza na vilabu vyao ili kuwashawishi."- Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments