Ticker

6/recent/ticker-posts

FIFA: Wydad Casablanca Kumlipa Saimon Msuva Sh 1.6 Bilioni

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

FIFA: Wydad Casablanca  Kumlipa Saimon Msuva Sh 1.6 Bilioni


BAADA ya kusubiri kwa miezi 7 hatimaye Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imlipe nyota wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva Dola za kimarekani 700,000 (zaidi ya Sh1.6 bilioni).

Familia Happygod Msuva ilipotafutwa imesema imemshukuru Mungu kwa kusikia kilio chao juu ya mtoto wao Msuva aliyeishtaki klabu hiyo FIFA kutokana na kushindwa kumlipa pesa za usajili sambamba na malimbikizo ya mshahara hatua iliyomfanya staa huyo kurejea nyumbani.

Baba wa Mchezaji huyo Happygod Msuva amesema tangu Novemba mwaka Jana walipoliwasilisha jambo hilo FIFA familia ilifunga kwa maombi na kumlilia Mungu.

"Familia tuliamua kumuachia Mungu hili jambo tukamwambia Mungu Kama haki ni ya kijana wetu itatendeka na kama ni ya Wydad basi itaonekana," amesema mzee Msuva.

Amesema baada ya kupata taarifa hiyo familia nzima iliangulia kilio cha furaha baada ya kuisubiri haki kwa muda mrefu.

"Yaani sasa hivi hakuna anayeweza kuongea sio Msuva, kaka, Mama wala dada yake wote wanamshukuru Mungu kwa kutenda," amesema.

Post a Comment

0 Comments