Ticker

6/recent/ticker-posts

Msuva Avunja Ukimya Kujiunga Yanga

Msuva Avunja Ukimya Kujiunga Yanga


Aliyekuwa mchezaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, Simon Happygod Msuva amesema anafahamu kuwa mashabiki wa Yanga wanataka arejee katika Klabu hiyo lakini yeye kwa sasa anatazama kucheza nje ya Tanzania kwanza.

Msuva jana ilitoka taarifa ya FIFA kuwa ameshinda kesi yake dhidi ya Wydad na wanatakiwa wamlipe pesa anazowadai kiasi cha Tsh bilioni 1.6.

“Mimi sikuondoka vibaya Yanga SC, najua wengi wanatamani nirudi Yanga SC. Sitaki kuwakatisha tamaa ipo siku nitarudi Yanga SC. Lakini kwa sasa bado natamani kucheza nje,” amesema Msuva.

Sasa Msuva yuko huru kujiunga na timu yoyote huku Yanga ikitajwa kumnyemelea staa wao aliyemaliza msimu wake wa mwisho Jangwani akiwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 14.

Post a Comment

0 Comments