Ticker

6/recent/ticker-posts

ZORAN MAKI KUSUKA UPYA BENCHI LA UFUNDI SIMBA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KOCHA Mkuu wa Simba, Zoran Maki amepewa jukumu zito la kulisuka Upya benchi la Ufundi la timu hiyo kwa ajili ya kufanya nao kazi.

Mabosi wa Simba wamempa kazi Zoran kutafuta wasaidizi wawili atakaokuja nao kwenye kambi ya timu hiyo itakayokuwa Misri kuanzia Julai 15 kwa maandalizi ya msimu mpya.


Katika kuhakikisha Simba inakuwa na benchi la ufundi imara, Zoran anatakiwa kutua Misri akiwa na wasaidizi wake wawili ambao ni kocha wa makipa pamoja na wa viungo.

Simba kwa sasa haina kocha wa makipa baada ya kuachana na Tyron Damons aliyepata kibarua kingine Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, huku pia ikiachana na kocha wa viungo, Mhispania Daniel De Castro.

Za ndani kabisa zinasema kuwa tayari ana majina mawili ya makocha atakaoenda nao kambini mmoja akiwa ni kocha wa makipa Mohamed Haniched aliyewahi kufundisha USM Blida, USM EL Harrach na USM Alger ambazo zote zinatoka nchini kwao Algeria.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza Zoran atakuja na kocha wa viungo anayetambulika kwa jina la Kareem Bayey ambaye anaelezwa amekuwa naye kwenye timu nyingi alizofundisha huko nyuma.

Zoran inaelezwa anavutiwa zaidi na kocha huyo wa viungo kwani mbali ya uwezo wake huo amekuwa pia akimsaidia kama kocha msaidizi ndio maana kila anapokwenda kufundisha anakuwa pamoja naye.

Mabosi wa Simba wamekubaliana na mapendekezo ya wasaidizi hao wa Zoran atakaokuwa nao kwenye kambi ya timu hiyo Misri. 

Post a Comment

0 Comments