Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za usajili: Man Utd wamgeukia Milinkovic-Savic; Juventus wamuhitaji Firmino

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Barcelona wanadai kuwa bado hawajakubali ofa yoyote kutoka kwa Manchester United au mtu mwingine yeyote kwa ajili ya Frenkie de Jong, na hivyo kupelekea klabu hiyo ya Old Trafford kumtazama Sergej Milinkovic-Savic wa Lazio kwa mara nyingine tena.

Liverpool wamewekewa ofa ya Euro milioni 23 mezani kutoka Juventus kwa ajili ya kumsajili Roberto Firmino, Juventus pia wanaiwinda saini ya Anthony Martial wa Manchester United licha ya Manchester United kutokuwa tayari kumuuza.

Manchester United wanamfuatilia kwa ukaribu kinda wa Red Bull Salzburg Benjamin Sesko, ingawa klabu hiyo ya Austria haipo tayari kumuuza kinda huyo msimu huu wa majira ya joto kwa chini ya €65m. Bayern Munich, Borussia Dortmund na Newcastle ni timu nyingine zinazomtaka Mslovenia huyo.

Memphis Depay ameambiwa na kocha mkuu wa Barcelona Xavi kwamba hamuhitaji tena Camp Nou.

Jules Kounde anaye windwa na Chelsea, yupo tayari kupokea ofa ya Barcelona wakati sakata lake na Chelsea likiwa linaendelea. Lakini The Blues wanaweza kulipiza kisasi kwa kuwazuia wababe hao wa Catalan kumsajili Cesar Azpilicueta.

Paris Saint-Germain wanatarajiwa kumsajili Nordi Mukiele kwa mkopo kutoka RB Leipzig kwa Euro milioni 15, jambo ambalo linaweza kumfungulia njia Presnel Kimpembe kuondoka klabuni hapo huku Chelsea na Juventus zikimuwania.

Kiungo wa kati wa Real Madrid, Casemiro anataka klabu hiyo kumsajili Neymar, ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Paris Saint-Germain.

Manchester City watamgeukia beki wa pembeni wa Stuttgart, Borna Sosa kama hawataweza kufanikisha dili la kumnunua beki wa Brighton, Marc Cucurella.

Arsenal wanavutiwa na kiungo wa Lyon Lucas Paqueta lakini bado hawajafanya mazungumzo yoyote. Wakati huo huo, Atalanta wana uhakika wa kumsajili beki wa kushoto wa Arsenal Nuno Tavares kwa mkopo.

Tottenham wako tayari kumuuza Tanguy Ndombele, ambaye anawindwa na miamba ya Uturuki Galatasaray.

Chelsea na Tottenham wamekuwa wakihusishwa na winga wa Newcastle Allan Saint-Maximin lakini hakuna anayetaka kulipa dau la pauni milioni £40m kumsajili.

Arsenal wamekataa ofa ya pauni milioni £10m kutoka kwa Fulham kwa ajili ya kumsajili mlinda mlango Bernd Leno, licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kukubaliana na The Cottagers. hata hivyo, Fulham wapo tayari kumgeukia kipa wa Barcelona Neto, ambaye anapendelea kuhamia Napoli.

Everton na Newcastle wanamtazama kinda wa Chelsea Armando Broja baada ya West Ham kujiondoa kutoka na kile kinachoonekana kushindwa makubaliano na Chelsea. The Hammers sasa wanamtazama mshambuliaji wa Blackburn na Chile Ben Brereton Diaz, huku dili la kumnunua mchezaji wa Sassuolo Gianluca Scamacca pia likishindikana.

Liverpool wanatarajiwa kumpeleka mlinzi chipukizi Sepp van den Berg kwa mkopo Bournemouth.

Everton wako tayari kumtoa Nathan Patterson kwa mkopo wa miezi sita baada ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland kwa mkataba ambao ulikuwa na thamani ya pauni milioni £16m.

Nottingham Forest inamtazama fowadi wa Burnley Maxwel Cornet, ambaye pia anawindwa na Fulham na Everton. Burnley wako tayari kutoa kiasi cha  pauni milioni £17.5m kama kifungu cha kwenye mkataba wake kinavyo sema.

Newcastle pia wanaweza kujaribu kumsajili winga Dwight McNeil kutoka Burnley , ambaye pia anavivutia vilabu vya Crystal Palace na West Ham.

Adrien Rabiot anafanya mazoezi na kikosi cha akiba cha Juventus huku akitarajia kuondoka katika klabu hiyo na kurejea Ufaransa, huku PSG au Lyon zikimvutia zaidi.

Post a Comment

0 Comments