Ticker

6/recent/ticker-posts

PSG iko tayari kumuuza Presnel Kimpembe kwa euro milioni 70

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KWA mujibu wa gazeti la The Times, mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain wanafikiria kumuuza Presnel Kimpembe kwa dau lisilo pungua euro milioni 70, huku Chelsea wakiwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumsajili mchezaji huyo.

Presnel Kimpembe amekuwa mmoja wa majina yanayozungumziwa sana linapokuja suala la Paris Saint-Germain katika wiki za hivi karibuni huku mwenendo wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ukitiliwa shaka kama atasalia PSG katika msimu huu wa majira ya joto.

Uwezekano wa kuwasili kwa Milan Skriniar PSG huenda ukafanya iwe vigumu kwake kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza na zaidi ya hayo, imesemekana kwamba haridhishwi na kiasi cha mshahara anacho lipwa kwa sasa.

Kimpembe hawezi kuguswa tena huko Paris, baada ya PSG kumweka sokoni huku ikihitaji kiasi cha euro milioni 70 ($70m) ili kumuuza, kama ilivyoripotiwa na The Times. Kutokana na dau hilo wanalohitaji PSG kwa timu inayo muhitaji mchezaji huyo,timu kadhaa kama Chelsea, Juventus na Atl├ętico Madrid wameonyesha nia kwamba wako tayari kupata huduma yake kwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwajili ya usajili.

Mchezaji huyo, hata hivyo, anataka kubaki. Kwa mujibu wa L’Equipe, tayari amekutana na uongozi wa PSG kuwafahamisha nia yake ya kuendelea kusalia klabuni hapo. Mkataba wake unaisha mnamo 2024 na, kwa sasa, hakuna taarifa kuhusu uwezekano wa kuongezwa tena mkataba.

Post a Comment

0 Comments