Ticker

6/recent/ticker-posts

Mashabiki wa Atletico Madrid waanza kampeni kwenye mitandao ya kijamii Kupinga usajili wa Cristiano Ronaldo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MASHABIKI wa Atletico Madrid wameanza kampeni kwenye mitandao ya kijamii kwa pamoja kueleza hasira zao kuhusu nia ya klabu hiyo kutaka kumsajili Cristiano Ronaldo.

Nyota huyo wa Ureno anatazamiwa kuondoka Manchester United msimu huu wa majira ya joto tangu mwaka mmoja tu kurejea kwake Old Trafford. Chelsea na Bayern Munich walikuwa wanamfuatilia lakini wamejiondoa katika kinyanganyiro hicho.

Ripoti kutoka Uhispania zinasema kwamba Atletico Madrid wanavutiwa kumsajili Ronaldo na wako tayari kumuuza Antoine Griezmann  ili kuweza kupunguza bili ya mshahara kwa ajili ya kufanikisha usajili wa Ronaldo. .

Hata hivyo, sawla hilo halijapokelewa vyema na baadhi ya mashabiki wa Atletico, ambao wanasisitiza kuwa klabu hiyo haipaswi kusajili mchezaji ambaye tamaduni zake zinahusiana sana na wapinzani wao Real Madrid.

Wafuasi wa Atletico wanatumia '#ContraCR7' - Ikimaanisha hawataki usajili 'dhidi ya CR7' - ili kufanya hisia zao kusikika. Hashtag imevuma sana nchini Uhispania mwishoni mwa wiki.

Ronaldo amecheza mechi nyingi dhidi ya Atletico kuliko timu nyingine yoyote katika maisha yake ya soka alipo kuwa Uhispania, akikutana na Los Rojiblancos mara 37 na kushinda 17 kati ya hizo.

Amefunga mabao 25 ​​dhidi yao (Sevilla pekee ndiyo amekuwa akiwafunga magoli mara nyingi zaidi), na alichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa ya 2014 na 2016 ya Real Madrid dhidi ya wapinzani wao(Atletico).

Hata hivyo, mara ya mwisho Atletico walifanikiwa kushinda pambano lao dhidi ya Man Utd na Ronaldo akiwemo na kufanikiwa kuwaondoa Man Utd kutoka Ligi ya Mabingwa katika hatua ya 16 bora msimu uliopita.


Post a Comment

0 Comments