Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili: De Jong nina furaha Barcelona; Ronaldo aifikiria Atletico

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa
Frenkie de Jong
amesema ana furaha kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha Barcelona msimu huu wa majira ya joto, lakini kama itambidi aondoke basi kiungo huyo angependelea kujiunga na Bayern Munich au Chelsea lakini sio Manchester United.

Chelsea wanakaribia kuinasa saini ya beki wa Sevilla, Jules Kounde, ambaye pia anawindwa na Barca, huku kocha Thomas Tuchel akipania kuimarisha safu yake ya ulinzi. Beki huyo anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya ndani ya saa 48 zijazo.

Chelsea pia wanavutiwa na chipukizi wa RB Leipzig Josko Gvardiol, ambaye anahitajika kuja kuchukua nafasi ya nahodha wa klabu hiyo Cesar Azpilicueta.

Cristiano Ronaldo atakuwa tayari kujiunga na Atletico Madrid kutokana na timu hiyo miamba hiyo kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hana wasiwasi na mshahara wake. Wakati huo huo, wapinzani wao Real Madrid hawana nia ya kumnunua tena Ronaldo msimu huu wa majira ya joto.

Man Utd bado wana mpango wa kumnunua mshambuliaji Antony wa Ajax, licha ya kwamba mpango huo ulisha kataliwa toka hapo awali na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Nchini Uholanzi.

Manchester City wameanza harakati za kuisaka saini ya beki wa pembeni Marc Cucurella, lakini bado hawaridhishwi na dau lililotajwa na Brighton kwaajili ya kumsaini beki huyo.

Iwapo Brighton watamuuza Cucurella, wanaweza kumchukua beki wa kushoto wa Arsenal Nuno Tavares kama mbadala wake.

Liverpool wanavutiwa na kiungo wa Borussia Monchengladbach Florian Neuhaus, ambaye wamekuwa wakihusishwa naye tangu dirisha la uhamisho lililopita.

Tottenham wapo tayari kumtoa Sergio Reguilon kwenda Barcelona kwa mkopo na La Blaugrana anaweza kuvutiwa ikiwa hawatakubaliwa kumnunua Marcos Alonso kutoka Chelsea.

Arsenal wamefufua nia yao ya kutaka kumnunua kiungo wa Juventus Arthur Melo, ambaye walimfuata bila mafanikio mwezi Januari.

Jesse Lingard amepewa mkataba wa awali wa miaka miwili na Nottingham Forest, huku Trees ikitarajia kuwashinda mahasimu wao West Ham ambao wamekuwa wakiwinda saini ya fowadi huyo kwa muda mrefu.

Forest pia wanafikiria kumnunua Emmanuel Dennis wa Watford, ambaye alifanya vyema msimu uliopita licha ya kushuka daraja kwa The Hornets.

Leicester City wamekataa kitita cha pauni milioni 15 kutoka Monaco kwa ajili ya kumnunua kiungo wao Boubakary Soumare, ambaye ameshindwa kuendana na kasi ya Ligi kuu ya Uingereza tangu alipo wasili kwenye klabu hiyo msimu uliopita wa majira ya joto.

Leicester City wana wasiwasi kuhusu fedha za Usajili hivyo wanatakiwa kuuza kwanza baadhi ya wachezaji kabla ya kuleta wachezaji wapya. Kwa sababu hiyo, wanafikiria kuachana na James Maddison, Kelechi Iheanacho au Timothy Castagne.

Rangers wanafikiria kumnunua beki wa kushoto wa Besiktas, Ridvan Yilmaz,huku wakiwa tayari wamemsajili Ben Davies ili kuimarisha safu yao ya ulinzi msimu huu.

Newcastle wametoa ofa ya pauni milioni 18 kumnunua winga wa Leeds United Jack Harrison, ambaye anaweza kuwa mchezaji wa pili kutegemewa kuondoka katika kikosi cha Leeds katika msimu huu wa majira ya joto.

West Ham na Everton wanachuana na vilabu kadhaa vya Ulaya kuwania saini ya Adnan Januzaj, ambaye kwa sasa mkataba wake unamalizika.

The Hammers pia wanavutiwa na winga wa Burnley Dwight McNeil, lakini Crystal Palace nao wako kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya winga huyo.

Post a Comment

0 Comments