Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba na Yanga Zategeana

Simba na Yanga zimeshindwa kuweka wazi hadi sasa ni lini yatafanyika matamasha yao ya kila msimu yale ya Simba Day na Siku ya Mwananchi.

Simba ndiyo ilianza kufanya tamasha la Simba Day mwaka 2009 na mara zote imekuwa na tamaduni ya kulihusisha na mashabiki, wadau na jamii nzima kwa ujumla na Baada ya kufanikiwa kwa misimu zaidi ya 10 huku kwa Yanga Wiki ya Wananchi raundi hii ikiwa kwa mara ya pili.


Tayari Simba imepaa kwenda kuweka kambi nchini Misri, huku Yanga ikijiandaa kwenda Uturuki au Arusha kwenye viwanja vya Black Rhino kukita kambi kule kwaajili ya kujifua kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na ligi nyingine za ndani zitakazoanza mwezi ujao lakini hadi leo hakuna timu iliyoweka wazi siku ya tamasha lao ni lini.

Wakati Akihojiwa ofisa habari wa Simba, Ahmed Ally alieleza kuwepo kwa tamasha hilo lakini bado tarehe rasmi haijapangwa.

“Tukirudi kutoka Misri kwenye tarehe za mwanzo wa mwezi ujao ndio tutafanya Simba Day, hadi sasa bado hatujaamua tarehe rasmi ni lini lakini mashabiki wetu wasiwe na hofu kabisa na siku si nyingi tutawatangazia lini tunafanya jambo letu hilo,” alisema Ahmed.

Kwa upande wa Yanga moja ya viongozi wa juu  ameeleza kuwa wanasubiri ratiba kamili ya maandalizi ya msimu ujao ‘pre season’ kutoka kwa kocha kisha watajua lini Wiki ya Mwananchi Ifanyike.

“Tunasubiri kujua mambo ya kambi yatakuaje maana tuna muda mchache na mambo ni mengi baada ya hapo mtafahamishwa,”.

Katika msimu uliopita Yanga ndiyo ilianza kufanya sherehe zake za Kilele cha Wiki ya Wananchi na kumalizika kwa mechi ya kirafiki dhidi Yan Zanaco na kupoteza kwa mabao 2-1 huku Simba Day ikifanyika Septemba 20 na kuhitimishwa kwa mechi dhidi ya TP Mazembe wenyeji Simba wakifa 1-0.

Katika nafasi nyingine Azam iliyopo mbioni kwenda Misri kukita kambi maalumu, imepanga kufanya tamasha lake la Azam Festival siku chache baada ya kurejea nchini mwezi ujao.

Post a Comment

0 Comments