Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba kuwa bora zaidi - Zoran Manojnlovic


Kocha mpya wa Simba, Zoran Manojnlovic leo amezungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaaam na kusema “Kila nchi ambayo nimewahi kufanya kazi kuna mechi za watani wa jadi, ili kufanya vizuri lazima kuwe na maandalizi ya kucheza mechi za aina hiyo”

“Nimepata mafanikio katika Timu mbalimbali ambazo nimewahi kufundisha, Simba ni Timu kubwa Tanzania na ni changamoto kwangu kwa mafanikio waliyopata Afrika hivyo kuna kazi ya kufanya”

“Nina taarifa kuhusu usajili wote ambao umekuwa ukifanywa na uongozi kwa ajili ya msimu mpya, nipo hapa kuifanya Simba kuwa bora zaidi ya msimu uliopita, mwaka huu ilimaliza nafasi ya pili, msimu ujao kuwa ya kwanza, msimu uliopita ilikuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na mwaka huu kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika”

Post a Comment

0 Comments