Ticker

6/recent/ticker-posts

Matthijs de Ligt Kutua Bayern Munich Muda Wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Bayern Munich wapo katika harakati za kukamilisha Uhamisho wa Mlinzi Matthijs de Ligt kutoka Juventus ya Italy.

Mholanzi huyo amekuwa akihusishwa kusajiliwa na vilabu vya Chelsea na Bayern katika miezi ya hivi karibuni, lakini kufuatia mazungumzo siku ya Jumatatu jijini Turin kati ya Hasan Salihamidzic na wakurugenzi wa Juventus, Inaonekana sasa huenda De Ligt akatua Bayern katika msimu huu wa majira ya joto.

Wakati wa kuondoka kwenye mazungumzo siku ya Jumatatu, mkurugenzi wa Bayern Salihamidzic, alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alisema: "Tutaona, siwezi kusema chochote kuhusu mkataba wa Matthijs de Ligt. lakini tuna matumaini".

Bayern Munich wanaamini kwamba Mlinzi huyo wa kati anapendelea kujiunga nao, baada ya kufurahishwa na namna wawakilishi wake walivyo mweleza mipango ya timu hiyo kwa sasa na hapo baadae chini ya mkurugenzi wa michezo Salihamidzic na kocha mkuu Julian Nagelsmann.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Kocha wa Juve, Max Allegri aligusia uwezekano wa kumuondoka kwa De Ligt akisema: "Kama mnavyojua jana kulikuwa na kikao na Bayern, lakini kwa sasa De Ligt bado ni mchezaji wa Juventus na anafanya mazoezi vizuri "

Huku kukiwa na Uwezekano mkubwa wa De Ligt kuhamia Bayern kuliko Chelsea, The Blues wameelekeza nguvu zao kwa nyota wa SSC Napoli Kalidou Koulibaly - na sasa wanapewa nafasi kubwa ya kumnasa Msenegali huyo mbele ya Juve - ambao wanamuhitaji Aje kuziba nafasi Inayoachwa wazi na De Ligt - huku wakiwa na mpango wa kusajili walinzi wakati watatu katika msimu huu wa majira ya joto.

Napoli tayari wamekamilisha mpango wa kumsajili Leo Ostigard kutoka Brighton kama mbadala wa muda mrefu wa Kalidou Koulibaly mwenye miaka 31 - Ostigard amewavutia maafisa wa Napoli wakati akichezea Genoa kwa mkopo msimu uliopita.

Post a Comment

0 Comments