Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba kuweka kambi nchini Misri

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


MSEMAJI wa klabu ya Simba, Ahmed Ally ameweka wazi timu yao kwenda kuweka kambi nchini Misri katika mji wa Ismailia kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hoteli ya Serena, Ahmed amesema safari ya kwenda Misri itaanza rasmi tarehe 14 Julai.


“Tunaondoa tarehe 14 mwezi huu na tutakuwa na tarehe tano mwezi wa nane tutarudi kwa ajili ya Simba Day pamoja na mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi,” amesema Ahmed na kuongeza;


“Tutakuwa na wachezaji wote kasoro wale ambao watakuwa kwenye timu za Taifa ambao tutawaacha wakiwa na majukumu mengine.”


Akizungumzia upande wa kocha wao mpya amesema wamempa mkataba wa mwaka mmoja na anatakiwa kuhakikisha Simba inapata ubingwa wa Ligi Kuu.


“Zoran yupo hapa kuhakikisha Simba inapata ubingwa wa Ligi, Ngao ya Jamii na Kombe la Shirikisho pamoja na kuingia nusu fainali Caf,” amesema Ahmed.

Upande wa kocha mpya wa Simba, Zoran Manojnlovic ni kama amepinga kauli hiyo baada ya kusema upande wake hataki kuahidi makubwa.


Zoran amesema jambo kubwa la kwanza ni kuhakikisha timu hiyo inafika hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.


“Sitaki kusema nitachukua ubingwa wa Afrika, mimi ahadi yangu ni kuhakikisha timu inafika hatua ya makundi halafu hatua zingine zinafuata.”


Zoran amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mwingine kulingana na mwenendo wa timu.

Post a Comment

0 Comments