Ticker

6/recent/ticker-posts

Silva Amtaka Neymar Chelsea

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

BEKI Thiago Silva wa Chelsea amemsihi Neymar ajiunge na klabu hiyo ya Stamford Bridge, iwapo ataamua kuachana na Paris Saint-Germain (PSG) msimu huu.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Ufaransa, tayari Neymar amejulishwa kwamba huduma zake hazitahitajika pale Le Parc des Princes msimu ujao.


Akizungumza kupitia kwa jarida la JG Brazil, Silva anaamini mshambuliaji huyo matata atakubali kujiunga na Chelsea msimu huu.

“Itakuwa bora sana iwapo atakubali kujiunga na Chelsea,” Silva alisema wakati wa mahojiano na jarida hilo.

“Iwapo atakubali ushauri wangu, atakuwa amefanya uamuzi utakaomfaidisha maishani kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa sielewi anachofikiria, lakini namtarajia afuate ushauri wangu.”

Juma lililopita, rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alimtumia ujumbe Neymar akisisitiza kwamba klabu yake haitamhitaji kwa siku sijazo.

“Pengine tubadilishe mwito wetu…lakini kwa sasa lazima tuambiane ukweli, wakati wa wachezaji kujipodoapodoa umekwisha, na sasa tunataka wachezaji halisi wa kusakata kandanda.”

Al-Khelaifi amesema hayo wakati mkataba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 na PSG unatarajiwa kumalizika 2025.

Wakati huo huo, muda mfupi tu baada ya kujiunga na Juventus, kiungo Paul Pogba amesema ameagana na Manchester United na kurejea Turin kwa lengo la kusaidia mabingwa hao kupata mataji.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, alitoka Juventus mnamo 2016 na kujiunga na Manchester United kwa mkataba uliogharimu zaidi ya Sh8 bilioni.

Lakini baada ya kuchezea Manchester kwa mara ya mwisho mnamo Aprili 19, ameondoka kama mchezaji huru, baada ya klabu hiyo kukataa kumpa mkataba mpya.

Lakini chini ya kocha Jose Mourinho alitatizika kiasi cha kupokonywa jukumu la kuwa naibu nahodha mnamo 2018, kabla ya nyota huyo kukumbwa na majeraha yaliyovuruga juhudi zake za kubaki kikosini cha kwanza.

“Nilikuwa hapa na nimerejea. Niko hapa kusaidia timu ishinde vikombe. Tutakuwa pamoja uwanjani kutimiza hii ndoto pamoja.”

Pogba aliondoka Juventus akiwa kijana, lakini amerejea akiwa mtu mzima. Mfransa huyo alijiunga na Manchester United akitokea kituo cha kunoa vipaji cha Le Havre akiwa na umri wa miaka 16 mnamo 2009, aliisaidia timu hiyo kutwaa mataji ya EFL Cup na Europa League.

Aliondoka baada ya kuifungia United mabao 16 msimu wa 2018-19, lakini kwa kipindi cha misimu mitatu iliyopita alifunga mabao manane pekee katika mechi 91, na moja tu kutokana na mechi 27.

Post a Comment

0 Comments