Ticker

6/recent/ticker-posts

Oliver Giroud Atua Tottenham

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Oliver Giroud Atua Tottenham

Oliver Giroud amehatarisha hasira za mashabiki wa Arsenal kwa kukiri kuwa alifikiria kujiunga na Tottenham alipokuwa akiichezea Chelsea.

Giroud alifichua kwamba alikuwa amekatishwa tamaa na maisha ya Chelsea chini ya Frank Lampard, uhamisho wa kwenda kwa wapinzani wao wa Arsenal ungekuwa sio vyema kwake.

Soma Pia | Tetesi za Usajili barani Ulaya

Lakini Giroud aliepushwa kufanya hatua hiyo yenye utata wakati AC Milan ilipokuja kupiga simu kuwa wanamhitaji.

Alisema:"Nilitamani sana kuondoka hata nilimwambia Lampard kwamba ningejiunga na Tottenham kwa sababu nilijua kuwa Jose Mourinho ananihitaji.

“Mwishowe, nadhani ingekuwa vigumu kwa sababu nilikuwa nimeichezea Arsenal.

"Hatima Yangu ilitaka niwe hapa leo, nivae T-shirt ya Rossoneri."

Post a Comment

0 Comments