Ticker

6/recent/ticker-posts

Erling Haaland azungumzia 'changamoto kubwa' Inayomkabili Man City

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland amekiri kwamba atakuwa na ‘changamoto kubwa’ kuzoea Ligi Kuu ya Uingereza na klabu yake mpya ya Manchester City  baada ya uhamisho wake wa majira ya kiangazi akitokea Borussia Dortmund Kukamilika.

City ilishinda kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Haaland mwezi Mei, na kufanikiwa kumsajili kwa dau la €60m, Haaland amefunga mabao 135 katika mechi 137 kwa ngazi ya klabu na nchi tangu kuanza kwa msimu wa 2019/20.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 tayari amecheza katika amecheza katika vilabu kadhaa vikiwemo vilabu kutoka katika taifa lake la Norway, Austria na Ujerumani, na sasa anajiandaa kucheza katika nchi ya nne  katika maisha yake.

"Ni changamoto kubwa," Haaland alisema, kupitia mtandao wa ManCity.com. "Ni nchi mpya, ligi mpya, kocha mpya ... kila kitu ni kipya. Ninajua jinsi unavyo kuja kwenye klabu mpya, nimefanya hivyo mara kadhaa hapo awali.”

Haaland ametambulishwa rasmi kuwa atavalia jezi nambari tisa kwa City baada ya kuondoka kwa Gabriel Jesus aliye kwenda Arsenal, huku meneja Pep Guardiola akiwa hana mshambuliaji wa kati anayefaa tangu mzee Sergio Aguero kuondoka katika klabu hiyo mnamo 2021.

Haaland ana imani na uwezo wake na yuko tayari kutulia kwa muda mrefu Manchester.

"Ilikuwa hatua kubwa kucheza Molde, Salzburg, Dortmund na sasa City," alisema. "Nimekuwa nikifikiria mambo mengi kila wakati. Nimesaini mkataba wa miaka mitano, hivyo inabidi nianzie hapo.


Post a Comment

0 Comments