Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili barani Ulaya

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Frenkie de Jong amekataa mpango wa kuhamia Manchester United katika majira haya ya kiangazi, kiungo huyo wa kati wa Barcelona ametoa sababu 10 kwa nini havutiwi na mabadiliko hayo.

Arsenal wapo tayari kufanya jaribio la kutaka kumsajili N'Golo Kante, ambaye aliachwa nje ya kikosi cha The Blues kwa ajili ya ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.

Raphinha ameshindwa kuvumilia amewapa Barcelona saa 48 kukubaliana na Leeds. Chelsea bado wanavutiwa na mshambuliaji huyo pia.

Man Utd wameambiwa na Ajax kuongeza ofa kwa Lisandro Martinez hadi €43m ikiwa wanataka kumsajili mlinzi huyo.

Licha ya kuwa na viungo wengi siku za hivi karibuni, United inasemekana imeshindwa kuwasilisha ombi la kumnunua mchezaji mwenza wa Martinez, Antony, hadi sasa katika dirisha hili la uhamisho.

The Red Devils wanakaribia kumsajili Thomas Strakosha kwa uhamisho huru kufuatia mlinda mlango huyo wa zamani wa Lazio kumaliza mkataba wake.

Juventus bado hawajapokea ofa madhubuti kwa ajili ya beki wao Matthijs de Ligt, ingawa Chelsea na Bayern Munich wanamuhitaji mchezaji huyo.

Aliyekuwa kipenzi cha Juve, Paulo Dybala bado hajapata timu, Man Utd inahusishwa na kutaka kumnunua Muargentina huyo.

Real Madrid wanatarajia kuachana na Dani Ceballos, Mariano Diaz na Marco Asensio kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho, baada ya kuondoka kwa Luka Jovic.

Brighton wanataka kumuongezea mkataba  Marc Cucurella huku kukiwa mabingwa wa Premier League Manchester City wakionyesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo.

Arsenal wapo tayari kumenyana na Seagulls katika harakati za kumsaka beki wa pembeni wa Benfica Alex Grimaldo.

Lucas Torreira anaweza salia Emirates msimu huu wa majira ya joto, baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha kocha Mikel Arteta kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.

Aston Villa wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa Uswizi Ludwig Augustinsson kutoka Sevilla. The Villans tayari wamemsajili Diego Carlos kutoka La Liga msimu huu wa majira ya joto.

Napoli wamethibitisha kuwa mshambuliaji wao wa muda mrefu Dries Mertens amekataa kuongeza mkataba ili kusalia katika klabu hiyo ya Serie A.

Newcastle wanafikiria kumnunua winga wa Leeds Jack Harrison msimu huu wa majira ya joto.

Mshambulizi wa Villarreal Arnaut Danjuma amegoma kuhamia West Ham.

Post a Comment

0 Comments