Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea wako mbioni kukamilisha Uhamisho wa Kalidou Koulibaly kutoka Napoli

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  •  Kalidou Koulibaly Mbioni kutua Chelsea
  •  Napoli wagoma kumuuza Juventus


Chelsea wana matumaini ya kukamilisha dili la kumnunua beki wa kati Kalidou Koulibaly, huku mchezaji huyo akitaka kuhamia London huku Napoli wakiwa hawataki kufanya biashara na wapinzani wao wa Serie A, Juventus.

Akiwa amejiunga na Napoli mwaka 2014, Koulibaly ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na sasa anajiandaa kwa changamoto mpya katika maisha yake mapya.

Chelsea wapo sokoni kusaka mabeki wa kati msimu huu wa majira ya joto baada ya kuwapoteza Antonio Rudiger na Andreas Christensen walio timkia Real Madrid na Barcelona kama wachezaji huru, wanaweza kusajili hata watatu ikiwa meneja Thomas Tuchel atakubali.

Kouliably anapewa kipaumbele, huku Chelsea ikiwasiliana na wakala wake mapema na mazungumzo ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 yanakwenda vizuri.

Maslahi binafsi hayatakuwa shida sana kati ya Chelsea na Mchezaji huyo kwa Sababu, Koulibaly ameonyesha nia kuelekea London.

Chelsea wanaongoza kinyanganyiro hicho kwa Sababu Napoli hawapo tayari kufanya biashara na Juventus. Kouliably Kuhamia Turin kungewezekana ikiwa Juventus ndio klabu pekee inayomtaka mchezaji huyo, lakini rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis yupo tayari kufanya biashara na Chelsea na ameweka wazi kuwa hataki kumuuza Koulibaly kwa Juventus.

Juventus wapo sokoni wanatafuta mbadala wa beki wa kati wa Uholanzi Matthijs de Ligt, ambaye Inaelezwa kuwa anakaribia kuhamia Bayern Munich - mabingwa hao wa Bundesliga wanazidi kuwa na uhakika wa kukamilisha dili hilo baada ya mazungumzo kwenda vizuri, hivyo kuzuia nia ya Chelsea kumuhitaji Mchezaji huyo. .

Chelsea inaonekana wameondoka kwa De Ligt na sasa klabu hiyo inamtaka Koulibaly na Nathan Ake wa Manchester City wawe mabeki wawili wa kwanza kati ya watatu wapya watakaowasili Stamford Bridge msimu huu wa majira ya joto.

Chaguo nambari tatu linabaki kwa Presnel Kimpembe wa Paris Saint-Germain au mlengwa wa muda mrefu Jules Kounde kutoka Sevilla.

Post a Comment

0 Comments