Ticker

6/recent/ticker-posts

Msola aacha alama Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Msola aacha alama Yanga

TULIANZA uongozi wetu Yanga ikiwa katika hali ngumu, hiyo ni kauli ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mshindo Msola.

Msola amesema alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti katika ukumbi wa Polisi Officers Mess alipoingia kuiongoza timu hiyo haikuwa na pesa. Amesema walilazimika kutoa pesa zao mifukoni kusafiri kwa nia njema ya kuitumikia Yanga.

"Wajumbe wangu hapo ni mashahidi Yanga ilikuwa na hali mbaya sana, tulipambana kama viongozi kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa".

"Miezi mitano ya mwanzo tulifanya kazi kwa wakati mgumu sana, tukamshukuru sana Mungu, GSM aliingia na kutusapoti," amesema Msola.

Ujio wa GSM ilikuwa Neema kubwa kwa timu na pumzi kwao viongozi kwa kuwa alisaidia kwa asilimia 100 usajili wa timu pamoja na kutoa Sh10 millioni bonasi kwa kila mechi.

Msola anasema amejivunia utawala wake alijitahidi kurejesha umoja ambao haikuwepo ndani ya timu hiyo.

"Nilikuta matawi machache lakini mpaka sasa naondoka madarakani Kuna matawi zaidi ya 700 ya Yanga naamini yataendelea kuongezeka," anasema Msola.

Post a Comment

0 Comments