Ticker

6/recent/ticker-posts

Habib Kyombo atua rasmi Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Habib Kyombo atua Simba rasmi

KLABU ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Habib Kyombo kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kutokea sintofahamu hapo awali.

Awali nyota huyo alidaiwa kusaini timu mbili tofauti akianza na wageni wa Ligi Kuu Bara Singida Big Stars kisha kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kukubali dili jipya la kujiunga na Simba.

Wakati akiitumikia Mbeya Kwanza katika msimu ulioisha Juni 29, mwaka huu staa huyo alifunga mabao sita ya Ligi Kuu Bara katika mechi 15 alizocheza na kikosi hicho ambacho  kimeshuka daraja baada ya matokeo mabovu.

Huu ni usajili wa kwanza Simba kwa wachezaji wazawa msimu huu baada ya ule wa Moses Phiri raia wa Zambia aliyejiunga na miamba hiyo Juni 15 akitokea klabu ya Zanaco ya huko nchini kwao Zambia.

Mbali na Usajili huo ila Mwanaspoti linafahamu nyota wengine ambao wamejiunga na miamba hiyo ni Victor Akpan kutoka Coastal Union, Cesar Manzoki (Vipers FC), Nelson Okwa (Rivers United) na Augustine Okrah aliyetokea Asante Kotoko.

Post a Comment

0 Comments