Ticker

6/recent/ticker-posts

Manara afichua siri nzito Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara ametangaza kwa wanachama wa klabu hiyo kwamba baada ya uchaguzi wa viongozi wao basi kutakuwa na sapraizi kubwa.


Manara ameyasema hayo wakati akisubili zoezi la kupiga kura lianze hali iliyofanya wanachama wa klabu ya Yanga kupiga shangwe.

Taarifa hiyo inachochea tetesi zinazoashilia wachezaji wao wapya akiwemo Aziz Ki kuja katika ukumbi huu wa mkutano wa uchaguzi.

Manara aliwageukia wagombea na kuwaambia mashabiki wa Yanga wanataka makombe na sio kitu kingine chochote.

“Nyie nendeni mkaijenge Yanga uwanjani, kiuchumi lakini wanachama wanataka makombe na sio kitu kingine kwani hiyo ndio furaha yao,” amesema Manara na kauli hiyo iliibua shangwe kutoka kwa wanachama.


Post a Comment

0 Comments