Ticker

6/recent/ticker-posts

Man Utd Wamuweka Cristiano Ronaldo Sokoni, Chelsea wajiandaa kutuma ofa

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Man Utd Wamuweka Cristiano Ronaldo Sokoni, Chelsea wajiandaa kutuma ofa


Manchester United wapo tayari kumruhusu mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo kuondoka  Old Trafford katika msumu huu wa majira ya joto, United wanategemea kupokea ofa kutoka kwa mahasimu wao wa Ligi Kuu (Premier League)  Chelsea Siku chache zijazo.

Uongozi wa United na kocha Erik ten Hag wote kwa pamoja walishitushwa na taarifa za Ronaldo pamoja wa wakala wake Jorge Mendes kuwa mchezaji huyo anaomba kuondoka Klabuni hapo.

Kocha Erik Ten Hag aliandaa mpango kambambe wa kumtumia Ronaldo kama muhimiri wake kuelekea msimu ujao, lakini baada ya Ronaldo kuomba kuondoka kocha huyo anambidi abadili mfumo kuelekea msimu ujao, huku Ronaldo mwenye miaka 37 akiamini ni muda sahihi wa yeye kuondoka na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Ronaldo Alirejea United akitokea Juventus, amefunga jumlaya mabao 24 katika mashindano yote katika msimu wake wa kwanza alipo rejea Old Trafford. Ronaldo Anaamini hawezi kupata changamoto Mpya kwa kuendelea kisalia United .

Kitendo cha United kushindwa kufudhu Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (Champions League) Kimepelekea Ronaldo Kufanya maamuzi hayo ya kuondoka, Manchester United nao wameweka wazi kuwa wanamruhusu Ronaldo kuondoka licha ya kwamba Amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa. 

Wakala Jorge Mendes anashughulikia Uhamisho wa mchezaji huyo na taarifa za kina ni kwamba Chelsea wapo tayari kutuma ofa.

Inaaminika kuwa United watamruhusu Ronaldo kuondoka kwa dau lisilo pungua pauni milioni 15, na klabu yoyote ambayo ipo tayari kumsajili ijiandae kumlipa mshahara usio pungua pauni laki nne £400,000-kwa wiki - Ingawa wakala  Mendes amesema timu itakayo kuwa tayari kumsajili mteja wake basi kiasi hicho cha mshahara kitapungua.

Chelsea chini ya kocha Thomas Tuchel wapo sokoni kutafuta washambuliji kwajili ya msimu ujao mbaka sasa wapo katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Raheem Sterling, kutoka Manchester city  na  Ronaldo pia anaweza akaungana nao muda si mrefu.

Wakati huo huo Bayern Munich wamejiondoa katika mbio za kumwania Ronaldo,lakini tajiri wa Paris Saint Germain nae ameonyesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo.


Post a Comment

0 Comments