Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba: Tunaanza kushusha wachezaji wapya

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


AFISA Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally; amewataka mashabiki wa timu hiyo kutulia na kusema muda si mrefu timu hiyo itaanza kushusha wachezaji wapya ambao tayari imewasajili.

Ahmed Ally amesema; “Tumeshamaliza kukisuka kikosi chetu. Wote tuliowahitaji wapo kwenye makaratasi yetu, muda si muda tutaanza kushusha vyuma.

“Al Ahly, Raja, Mamelod, Mazembe, Zamalekh, Wydad wanasubiri kwa hamu kuona tumesajili nani maana tutakutana nao kwenye Makundi ya Klabu bingwa Afrika Insha Allah.

“Mashabiki wa Simba SC kuleni Sabasaba kwa amani, kuleni Eid vizuri mwenye kuchinja na achinje na baada ya hapo mtafurahi…” alimaliza kwa kusema hayo.

Post a Comment

0 Comments