Ticker

6/recent/ticker-posts

Man United Wamtaka Ronaldo Kurejea Kambini Au Kuondoka

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Man United Wamtaka Ronaldo Kurejea Kambini Au Kuondoka




KOCHA Erik ten Hag amemtaka Cristiano Ronaldo hadi mwisho wa wiki hii awe amejiunga na wenzake kambini au la, amteme katika kikosi cha mabingwa hao mara 20 wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Man United kwa sasa wapo jijini Bangkok, Thailand wakijiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza na wanategemea kupimana nguvu na Liverpool usiku wa Julai 11, 2022 kabla ya kuelekea Australia kwa mechi zaidi za kirafiki dhidi ya Melbourne Victory mnamo Julai 15, 2022 kisha Crystal Palace na Aston Villa.

Mwanzoni mwa Julai 2022, Ronaldo, 37, aliwataka Man United kumwachilia aondoke  Old Trafford. Mreno huyo ambaye sasa anajifanyia mazoezi jijini Lisbon, alirejea Man United mwanzoni mwa msimu wa 2021/22 baada ya kukatiza uhusiano na Juventus waliomsajili kutoka Real Madrid ya Uhispania kwa mkataba wa miaka minne.

Aliibuka mfungaji bora wa Old Trafford mnamo 2021/22 na kuambulia nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora wa EPL kwa mabao 18 nyuma ya Son Heung-min (Tottenham Hotspur) na Mohamed Salah (Liverpool).

Mbali na Real waliowahi kujivunia maarifa ya Ronaldo kati ya 2009 na 2018, klabu nyinginezo zinazowania huduma za Ronaldo ni AS Roma, Bayern Munich, Paris Saint-Germain (PSG) na Sporting Lisbon. 

Kuondoka kwa Ronaldo ambaye ni mchezaji anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa zaidi katika EPL – akikunja kiasi cha £480,000 kwa wiki – kutapunguza gharama ya matumizi ya fedha ya Man United na kumpa Ten Hag fursa ya kujishughulisha zaidi katika soko la uhamisho kadri anavyolenga kukisuka upya kikosi chake.

Kufikia sasa, Man United wamemsajili Tyrell Malacia kwa mkataba wa miaka minne baada ya beki huyo kuondoka Feyenoord ya Uholanzi kwa  £14.7m. Wanatarajiwa pia kujinasia huduma za Christian Eriksen wa Brentford, Frenkie de Jong wa Barcelona na wanasoka watatu wa Ajax – Jurrien Timber, Antony Matheus na Lisandro Martinez.

Post a Comment

0 Comments