Ticker

6/recent/ticker-posts

Ajax yaongeza dau kwa Man Utd Sasa Inahitaji €140m kwajili ya Antony & Lisandro Martinez

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Ajax wameongeza dau kwajili ya Mlinzi wao wa kati Lisandro Martinez anayetakiwa na Manchester United hadi €60m huku mazungumzo kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo kati ya pande hizo mbili yakiendelea.

United wametuma ofa mbili kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, anayemudu kucheza kama beki wa kati lakini pia anaweza kucheza beki wa kushoto na kiungo mkabaji, United wamemfanya Martinez kuwa chaguo lao nambari moja katika safu ya ulinzi katika wiki za hivi karibuni kutokana na Erik ten Hag kutaka kumsajili mchezaji huyo. 


Wawakilishi wa Martinez walikuwa wameihakikishia United kwamba dau la €50m linatosha kumngoa Mlinzi huyo kutoka kwa mabingwa hao wa Uholanzi - United wamefikisha kiwango hicho cha ofa lakini Ajax wameongeza dau zaidi kwajili ya mchezaji huyo.

Mlinzi huyo amekasirishwa na kitendo cha timu yake ya Ajax kuongeza dau, anahisi ofa ya hivi punde ya United ni sahihi, sasa inasalia kuona ni wapi atakwenda ikiwa makubaliano yatafanyika. Arsenal walikuwa wa kwanza kutuma ofa wakimuhitaji mlinzi huyo wa kati, lakini kwa sasa wamepunguza kasi ingawa bado wana nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

Kamati ya Usajili ya United kwa muda mrefu imekuwa ikimuhitaji Pau Torres wa Villarreal, ambaye anaweza kupatikana kwa takriban pauni milioni 45 katika msimu huu wa majira ya joto, ingawa Ten Hag anatafuta kusajili wachezaji wanaofahamu aina yake ya uchezaji wake katika msimu wake wa kwanza wa kuinoa United. Hapo awali Martinez alisajiliwa na Ten Hag akiwa kocha wa Ajax misimu mitatu iliyopita ya majira ya joto na amecheza zaidi ya mechi 100 tangu wakati huo.

Winga wa kulia wa jax Antony anahitajika sana na Ten Hag, United ipo kwenye mazungumzo kwajili ya wachezaji wote wawili lakini Ajax wanahitaji kiasi kisicho pungua €140m (sawa na £120m) ambacho ni zaidi ya kiasi ambacho walikusudia kulipa tangu awali.

Wote Antony na Martinez wanahitaji kuondoka, lakini jukumu hilo lipo kwa vilabu kukubaliana ada kwajili ya uhamisho wao.

Kwingineko, United wanakaribia kumsajili Christian Eriksen na wanamatumaini kwamba anaweza kuungana nao katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa kiangazi nchini Australia.

Post a Comment

0 Comments