Ticker

6/recent/ticker-posts

Metacha atambulishwa Singida Big Stars

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KIPA wa timu ya Taifa Ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Metacha Mnata ametangazwa kusajiliwa na klabu ya Singida Big Stars ‘SBS’ kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Polisi Tanzania FC.

Metacha ametambulishwa rasmi leo kupitia kurasa ya mtandao wa kijamii wa Instagram wa SBS timu iliyopanda Ligi Kuu na kubadilishwa jina ikitokea Championship ilipokuwa ikiitwa DTB.


Katika siku za hivi karibuni, Metacha amekuwa na muendelezo mzuri wa ubora ndani ya kikosi cha Taifa Stars akiwa chaguo la pili la kocha mkuu Kim Poulsen nyuma ya Aishi Manula wa Simba na alikuwa kipa namba moja wa Polisi kwa msimu uliomalizika.

Kipa huyo pia katika nyakati tofauti kabla ya kutua Polisi msimu uliopita, aliwahi kuzidakia timu za Azam (iliyomkuza), Mbao na Yanga.

Utambulisho wa Metacha ndani ya SBS unakuwa wa tano tangu ianze kusajili wachezaji wapya kwaajili ya msimu ujao na hapo awali iliwatambulisha mabeki, Paul Godfrey ‘Boxer’ kutokea Yanga na ‘AbdulMajid Mangalo aliyekuwa nahodha wa Biashara United.

Wengine ambao tayari wametambulishwa na SBS ni kiungo Aziz Andambwile kutokea Mbeya City na Mshambuliaji Kelvin Sabato ‘Kiduku’ aliyekuwa Mtibwa Sugar msimu ulioisha.

Singida inaendelea na usajili wa wachezaji wapya ili kuhakikisha inafanya vizuri kwenye Ligi Kuu na mashindano mengine kwa msimu wa 2022/2023.

Post a Comment

0 Comments