Ticker

6/recent/ticker-posts

Joyce Lomalisa Mutambala atua yanga rasmi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Joyce Lomalisa Mutambala atua yanga rasmi
  • Apewa mkataba wa miaka miwili
YANGA SC imekamilisha usajili wa beki raia wa DR Congo, Joyce Lomalisa Mutambala na kumpa mkataba wa miaka miwili, huku kwa mwezi akitarajiwa kulipwa shilingi milioni sita.

Kwa muda wa miaka miwili akiwa anaitumikia Yanga, jumla atakuwa amepokea mshahara wa shilingi milioni 144 hadi kumalizika kwa mkataba wake.

Mutambala anajiunga na Yanga akitokea Bravos do Maqui ya Angola, pia amewahi kucheza GD Interclube (Angola), AS Vita (DR Congo) na Mouscron ya Ubelgiji.

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga, kimethibitisha kwamba, Mutambala alikuwa hapa nchini kwa takribani wiki moja kukamilisha usajili wake.

“Naomba nikueleze kuwa, kuna uwezekano mkubwa sana kwa Kocha Nasreddine Nabi kuwaondoa kwa mkopo mabeki wa kushoto, David Bryson na Yassin Mustafa kwa sababu tayari dili la beki wa kimataifa raia wa DR Congo, Lomalisa Mutambala limekamilika.

“Mutambala alikuja nchini akasaini mkataba wa miaka miwili, kisha akaondoka. Atakuwa akilipwa mshahara wa shilingi milioni 6.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Saidi, hivi karibuni alisema wamepanga kufanya usajili mkubwa kuiandaa timu hiyo ili ifanye vizuri katika michuano ya kimataifa na ile ya ndani kwa msimu ujao wa 2022/23.


Post a Comment

0 Comments