Ticker

6/recent/ticker-posts

Zoran amleta Mohamed Ouattar Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KOCHA Mpya wa Simba Zoran Maki ameutaka uongozi wa timu hiyo uachane na beki wa kati kutoka St George ya Ethiopia, Mghana Edwin Frimpong, kwa vile anaye beki wa kati mkali aitwaye Mohamed Ouattar aliyefanya naye kazi katika klabu alizowahi kuzinoa Afrika ya Kaskazini na mabosi hao wamemwelewa na sasa ni suala la muda tu kabla ya kuja.

Inaelezwa mara baada ya kusaini mkataba wa kuinoa Simba, Zoran alielezwa kikosi kina shida ya beki wa kati baada ya kuachana na Pascal Wawa na walikubaliana wamchukue Frimpong aliye kwenye ubora kwa sasa kule Ethiopia.

Hata hivyo, Zoran aliwaeleza viongozi hao wa Simba kuachana na Mghana huyo ili amvute beki wa kati wa Al Hilal inayoshiriki Ligi Kuu ya Sudan, Mohamed Ouattara (29) raia wa Burkina Faso.

Inadaiwa Zoran aliwaambia viongozi hao wa Simba ana uhakika na kiwango bora cha Ouattara, kwani amewahi kufanya nae kazi katika klabu mbili tofauti na zote alikuwa akimtumia katika kikosi cha kwanza akianza naye Wydad Casablanca kisha Al Hilal.

Zoran aliwaambia kwa aina ya timu hizo mbili zilivyo isingekuwa rahisi kwa mchezaji kucheza kikosi cha kwanza bila ya kuwa na kiwango bora na mabosi hao wamemuelewa na fasta wakaanza mazungumzo na Ouattara ili aungane na timu hiyo kambini nchini Misri..

Chanzo makini kutoka ndani ya Simba kinasema, katika mazungumzo yao na Ouattara, beki huyo alitaka mzigo mnene, kitu kilichowatisha mabosi hao, lakini baada ya ushawishi wa Zoran inaelezwa amekubaliana na sasa ni suala la muda tu beki huyo kutua Simba.

“Kama itatokea hawataridhika na chaguo hilo la kocha Zoran, basi kuna uwezekano mkubwa kwenye dirisha dogo mabosi wa Simba wakarudi tena kwa Frimpong ambaye ndiye chaguo lao, lakini aking’ara maana yake dili la Mghana litakuwa limekufa rasmi.

Simba ikifanikiwa kukamilisha dili hilo, beki huyo ataungana na wengine wanne waliopo kikosini akiwamo Henock Inonga (beki Bora wa Ligi Kuu 2021-2022, Joash Onyango, Kennedy Juma na Erasto Nyoni.

Pia itakuwa imefunga dirisha la usajili kwani tayari mikononi mwao wana Moses Phiri, Habib Kyombo, Cecar Manzoki, Nelson Okwa, Augustine Okrah, Victor Akpan, aliyetambulishwa rasmi jana na klabu hiyo na Nassor Kapama anayetarajiwa kutambulishwa leo.

Post a Comment

0 Comments