Ticker

6/recent/ticker-posts

Harry Maguire Kuendelea Kuwa nahodha Manchester United

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Harry Maguire Kuendelea Kuwa nahodha wa united


KOCHA wa Manchester United Erik ten Hag amethibitisha kuwa Harry Maguire ataendelea kuwa unahodha wa united kwa msimu wa 2022/23.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikabidhiwa kitambaa na meneja wa zamani Ole Gunnar Solskjaer Januari 2020 - miezi sita tu baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa dau la £80m akitokea Leicester City - kufuatia Ashley Young kuhamia Inter.

Baada ya msimu wa kuvutia wa 2020/21 na kampeni bora zaidi ya Euro 2020 akiwa na England, Maguire alionekana kuwa amewanyamazisha wanaomtilia shaka.

Hata hivyo, alikuja kukosolewa vikali kwa uchezaji wake katika msimu mbaya wa 2021/22 wa Man Utd ambapo walimaliza na jumla ya pointi chache zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Mwaka jana Maguire angeweza kuvuliwa unahodha na bosi wa muda Ralf Rangnick, lakini Mjerumani huyo aliamua kupinga wazo hilo.

Ten Hag akihojiwa kuhusu mipango yake ya kitambaa cha Unaodha katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Thailand na  Australia,alisema kwa ufupi kwa nini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ataendelea kama nahodha.

"Harry Maguire ndiye nahodha," alisema. "Lazima niwafahamu wachezaji wote, lakini yeye ni nahodha imara na amepata mafanikio mengi."

Post a Comment

0 Comments