Ticker

6/recent/ticker-posts

Erik ten Hag Asisitiza Cristiano Ronaldo hauzwi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  •  Erik ten Hag Asisitiza kwamba Cristiano Ronaldo hauzwi


KOCHA wa Manchester United Erik ten Hag amesisitiza kwamba Mshambuliaji wao raia wa Ureno Cristiano Ronaldo hauzwi licha ya mchezaji huyo kuomba kuondoka Klabuni hapo katika msimu huu wa majira ya joto.

Ten Hag, akizungumza katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kabla ya mechi yao na Liverpool kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya nchini Thailand siku ya Jumanne, Kocha huyo alipokea maswali mengi kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 na mustakabali wake Old Trafford....... Ronaldo alijiunga tena na United msimu uliopita majira ya joto lakini tangu arejee klabu hiyo iliambulia kumaliza msimu vibaya, kubadilisha makocha na kumaliza nafasi ya sita kwenye Ligi.

Licha ya wawakilishi wa Ronaldo kuweka wazi wiki za hivi karibuni kuhusu nia ya mchezaji huyo kutaka kuondoka United kwa ajili ya kucheza Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao, uwezekano wa mchezaji huyo kuondoka ni mdogo na United wameweka wazi nia yao ya kuendelea kumuhitaji.

Ten Hag amekaririwa akiyasema hayo mara kadhaa alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari, na kukiri kuwa masuala binafsi ndiyo yamesababisha Mshambuliaji huyo kutokuwepo kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya, ambapo United itakwenda hadi Australia.

"Hayupo nasi kutokana na masuala binafsi," Ten Hag alisema. "Tunampango na Cristiano Ronaldo kwa msimu huu na ndivyo hivyo. Natarajia kufanya naye kazi .

"Sijui [jinsi ya kumfurahisha], hajaniambia hili. Lakini Cristiano Ronaldo hauzwi, yuko katika mipango yetu na tunataka kupata mafanikio pamoja."

Ten Hag amekiri kuwa amezungumza na Ronaldo tangu ateuliwe kuwa kocha, lakini akaweka wazi kuwa hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika baina yake na mshambuliaji huyo tangu habari za kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo zilipoibuka mwishoni mwa mwezi uliopita.

"Nilizungumza naye, lakini kabla ya suala hili kutokea," aliongeza. "Tulikuwa na mazungumzo mazuri, lakini hiyo ni kati yangu na Cristiano Ronaldo.

"Siwezi kuwaambia [kama Ronaldo atajiunga na ziara ya maandalizi ya msimu mpya] kwa sababu ambazo tayari nimezieleza."

Ten Hag amethibitisha kuwa klabu hiyo inaendelea na harakati za "Usajili" katika eneo la kiungo na ushambuliaji.


Post a Comment

0 Comments