Ticker

6/recent/ticker-posts

KAPAMA ATUA SIMBA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa Kiungo nyota Nassoro Kapama Kutoka Kagera Sugar kwa Mkataba wa Miaka miwili.


KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo nyota Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Kapama ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi ndani ya kiwanja ikiwemo beki, kiungo na nafasi ya ushambuliaji hali iliyowavutia benchi la ufundi la Simba.

Kwa msimu uliopita Kapama akiwa Kagera Sugar amecheza mechi 25, akifunga mabao mawili na kutoa pasi za magoli 3 (assist tatu)

Simba imeendelea kuimarisha safu yao ya kiungo kuelekea msimu mpya wa mashindano, wekundu hao wa msimbazi inatarajiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari Klabu ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya nyota wengine kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Moses Phiri mshambuliaji kutoka Zanaco ya nchini Zambia, Kiungo mkabaji Victor Akpan kutoka Coastal Union pamoja na Habibu Kyombo ambaye alivunja mkataba wake na Singida Big Stars kabla ya kujiunga na Simba.

Post a Comment

0 Comments