Ticker

6/recent/ticker-posts

Djuma Shabani Aongeza mkataba Yanga hadi 2024

Djuma Shaban asalia Yanga kwa mwaka mmoja Zaidi

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya soka ya Yanga, imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake wa kulia Raia wa Congo, Djuma Shabani ambao unamfanya aendelee kusalia ndani ya kikosi hicho hadi 2024.

Mchezaji huyo ameongeza mkataba leo mara baada ya kurejea ndani ya kikosi hicho akitoka mapumzikoni.

Mkaba wa awali wa mchezaji huyo ulikuwa unamalizika kwenye msimu ujoa ambao unatarajia kuanza hivi karibuni, kufuatia kusaini miaka miwili hapo awali.

Tangu alipo sajiliwa 2021, akitokea klabu ya AS Vita, Djuma amekuwa na msimu mzuri akiwa Yanga na alifanikiwa kuibuka kuwa kinara wa utoaji wa pasi za mwisho (assist).

Pia alifanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha msimu, katika tuzo zilizotolewa na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) tarehe 7 julai 2022.
Post a Comment

0 Comments