Ticker

6/recent/ticker-posts

Cristiano Ronaldo Athibitisha Kurejea mazoezini Man Utd

Cristiano Ronaldo Athibitisha Kurejea Mazoezini na Man Utd


Cristiano Ronaldo ameweka picha kwenye mitandao ya kijamii kuthibitisha kuwa amerejea tena mazoezini na Manchester United.

Mshambuliaji huyo hajashiriki katika mechi za Man Utd za kujiandaa na msimu mpya baada ya kupewa muda wa kuwa nje ya timu kutokana na masuala yake binafsi.

Ronaldo alikosa ziara ya Man Utd ya kujiandaa na msimu mpya nchini Thailand na Australia na mara kadhaa amekuwa akijaribu kuomba kuondoka ili akajiunge na timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa.

Ronaldo mwenye miaka 37 nia yake ni kuondoka Old Trafford, lakini klabu hiyo inataka kumbakisha na  meneja mpya Erik ten Hag amesisitiza kwamba bado ana mipango nae kwa msimu mpya.

Mchezaji huyo alithibitisha Ijumaa kwamba kuna uwezekano akarejea uwanjani katika mechi ya kirafiki siku ya Jumapili dhidi ya Rayo Vallecano katika dimba la Old Trafford , na kuweka picha kwenye Instagram Jumamosi kuonyesha kwamba amerejea tena mazoezini.


Alipiga picha ya pamoja na Charlie McNeill, Amad Diallo, Charlie Savage na Hannibal Mejbri, huku kikosi cha Man Utd dhidi ya Rayo Vallecano kikitarajiwa kuwa na wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza pamoja na vijana.

Wachezaji wengi tegemeo la Kocha Erik Ten Hag wamecheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Atletico Madrid na kushuhudia Man Utd ikichapwa 1-0 mjini Oslo. Joao Felix alifunga bao lililoipa ushindi Atletico katika dakika za mwisho na Fred akatolewa nje kwa kadi nyekundu, huku Kiungo Christian Eriksen akicheza mechi yake ya kwanza akitokea benchi. 

Post a Comment

0 Comments