Ticker

6/recent/ticker-posts

Cristiano Ronaldo awasili Manchester kwa mazungumzo juu ya mustakabali wake klabuni hapo


Cristiano Ronaldo na wakala wake Jorge Mendes wamewasili katika uwanja wa mazoezi wa Manchester United wa Carrington kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mustakabali wa fowadi huyo.

Ronaldo hakuweza kusafiri na wachezaji wenzake kwa ajili ya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya kwa 'sababu za kifamilia', ingawa kabla ya hapo alikuwa ameitaarifu klabu kwamba anataka kuondoka katika msimu huu wa majira ya joto.

Inaelezwa kwamba msimamo wa Ronaldo bado haijabadilika nia yake ni kutaka kuondoka, huku wakala wake Jorge Mendes akiendelea kutafuta klabu inayo shiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ajili ya mteja wake.

Chelsea na Bayern Munich zirihusishwa siku za nyuma kumuhitaji mshambuliaji huyo lakini kwa sasa, anahusishwa zaidi kuhamia kwa mahasimu wake wa zamani Atletico Madrid kwa siku za hivi karibuni.

Leo asubuhi, Ronaldo na Mendes walipigwa picha wakiwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa United kabla ya mazungumzo kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo. Ripoti kutoka vyanzo mbalimbali vinadai kuwa meneja wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson nae amesafiri kuelekea Carrington.


Post a Comment

0 Comments