Ticker

6/recent/ticker-posts

Matola: Simba ya msimu Ujao Itakuwa tishio

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Matola: Simba ya msimu Ujao itakuwa tishio


KOCHA Msaidizi wa Simba Seleman Matola, ameupongeza uongozi pamoja na Kamati ya Usajili kwa kufanya usajili ambao umeziba mapungufu yote yaliyokuwepo msimu uliopita.

Matola amesema kwa sasa kila namba kikosini ina wachezaji bora zaidi ya mmoja hivyo imeongeza ushindani mkubwa mazoezini kila mmoja anajitahidi kulishawishi benchi la ufundi.

Matola pia ameupongeza uongozi kwa kumleta Kocha Zoran Maki ambaye falsafa zake zinaendana na timu hivyo imekuwa rahisi wachezaji kuelewa anachofundisha.

“Leo ni siku ya 11 tangu tulivyoanza kambi yetu hapa Misri, jambo zuri ni kwamba imekuwa rahisi kwa wachezaji kuelewa mafunzo ya kocha na hii inatosha kusema falsafa yake inaendana na timu.

“Niupongeze uongozi kwa kufanya usajili mzuri pamoja na kumleta kocha Zoran. Mimi niwahakikishie tu wanasimba kwamba msimu ujao tutakuwa na timu imara ambayo kila Mwanasimba ataifurahia,” amesema Matola.


Post a Comment

0 Comments