Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili: Kounde anakaribia kujiunga Barca; Ronaldo arejea Manchester kuomba uhamisho

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Cristiano Ronaldo
amerejea Manchester kwa mazungumzo ya ana kwa ana na meneja mpya wa Manchester United Erik ten Hag, fowadi huyo anatazamiwa kuomba ruhusa ya kuihama klabu hiyo mara moja.

Chelsea wanahofia kuwa Jules Kounde atakataa nafasi ya kuhamia Stamford Bridge msimu huu wa majira ya joto na badala yake atajiunga na Barcelona.

The Blues baada ya kuzidiwa ujanja na kumpoteza Jules Kounde kwa Barcelona sasa wanampango wa kuwazuia wachezaji wao Cesar Azpilicueta na Marcos Alonso kujiunga na wababe hao wa Catalan.

Liverpool wanamfuatilia winga wa Athletic Club Nico Williams, ambaye ni mdogo wake Inaki Williams. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 20 tayari ana thamani ya zaidi ya £40m.

Real Madrid, Barcelona na PSG wako tayari kuchuana na vilabu vikubwa vya Premier League kwa ajili ya kuinasa saini ya kinda wa Palmeiras Endrick.

PSG wanajiandaa kupokea ombi kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya kumsajili fowadi Julian Draxler. Mabingwa hao wa Ligue 1 wapo tayari kumuuza mshambuliaji huyo kwa £17m.

Leeds United na Everton zote zimepewa nafasi ya kumsajili beki wa kushoto wa PSG Layvin Kurzawa.

Mshambulizi wa Real Madrid Borja Mayoral yuko mbioni kujiunga na Getafe kwa ada ya €10m.

Arsenal wamepewa nguvu katika harakati zao za kumnasa Lucas Paqueta, baada ya Lyon kuonyesha kuwa wapo tayari kupokea maombi kwa klabu yeyote inayo hitaji kumnunua kiungo huyo.

Nia ya Tottenham kumuhitaji Nicolo Zaniolo wa Roma inaendelea, ingawa Juventus wanatazamiwa kushindana nao kwa ajili ya huduma yake.

West Ham wamekataa mpango wa Fulham kwa Issa Diop.The Cottagers hawapo tayari kupokea chini ya pauni milioni £15m kama ada ya uhamishao wa mchezaji huyo kwa timu yeyote inayo muhitaji.

Kocha wa Barcelona Xavi amemjulisha Memphis Depay kutafuta klabu mpya msimu huu wa majira ya joto, kwani haoni mustakabali wake akiwa Barcelona.

Inter wanampango wa kuachana na mshambuliaji Alexis Sanchez analyelipwa mishahara mkubwa klabuni hapo, Mchile huyo anaweza kushtukiza na kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Marseille.

Newcastle wana nia ya kumsajili Harvey Barnes, lakini Leicester wamesema hauzwi katika msimu huu wa majira ya joto.

The Foxes wanaweza kumruhusu nahodha wa klabu hiyo Kasper Schmeichel kuondoka msimu huu wa majira ya joto huku mkataba wa mlinda mlango huyo wa muda mrefu ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Nice pia wanavutiwa na kipa huyo.

Southampton wanamatumaini ya kuwashinda Bayer Leverkusen katika mbio za kumnasa winga chipukizi wa Manchester City Sam Edozie.

AC Milan wako tayari kuongeza dau kwa Charles De Ketelaere huku wakijaribu kuharakisha kupata saini ya mchezaji huyo wanae muhitaji kwa muda mrefu. Leeds na Leicester pia wanavutiwa na mshambuliaji huyo.

The Rossoneri pia wanafikiria kumnunua mchezaji wa Chelsea Hakim Ziyech pia, huku raia huyo wa Morocco akifikiria kuondoka.

Post a Comment

0 Comments