Ticker

6/recent/ticker-posts

Cristiano Ronaldo athibitisha kurejea Man Utd

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Cristiano Ronaldo ameweka wazi kwamba anajipanga kurejea dimbani siku ya Jumapili ambapo kikosi cha Manchester United kitakuwa na mchezo dhidi ya Rayo Vallecano.

Fowadi huyo amekosa mechi zote za maandalizi ya msimu mpya wa Man Utd hadi sasa baada ya kupewa likizo kutokana na matatizo ya kifamilia, ingawa anataka kuhama Old Trafford na kwenda kwenye timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man Utd kupitia tovuti yao wamethibitisha kwamba siku ya Ijumaa Ronaldo hatosafiri na kikosi kitakachomenyana na Atletico Madrid nchini Norway Jumamosi.

TAZAMA HAPA JEZI MPYA ZA YANGA 2022-2023

Kupitia Akaunti ya Instagram ya shabiki Man Utd yaliwekwa majina 21 ya wachezaji wa kikosi kitakacho chuana na Atletico, ambapo Ronaldo alitoa maoni yake kwa kusema 'Sunday the king plays' akimaanisha "Jumapili, mfalme anacheza".

Baada ya kumenyana na Atletico siku ya Jumamosi, Man Utd watarejea Old Trafford kumenyana na Rayo Vallecano kesho yake mchana.

Erik ten Hag, ambaye atasimamia mechi yake ya kwanza ya nyumbani tangu achukue mikoba ya Ralf Rangnick, anajaribu kukiandaa kikosi chake na mchezo wa mwishoni mwa juma kabla ya kurejea kwa Ligi Kuu wiki ijayo.

Man Utd wataanza kampeni yao wakiwa nyumbani kwa Brighton Jumapili ijayo, kabla ya kusafiri kuelekea magharibi mwa London kumenyana na Brentford Jumamosi inayofuata.

Jaribio la kwanza kubwa kwa kocha Ten Hag litakuwa siku ya Jumatatu Agosti 22 wakati Liverpool watakapotembelea Old Trafford kuwakabili Man Utd. Mara ya Mwisho Man Utd walipo kutana na Liverpool Vijana wa Jurgen Klopp walishinda 5-0.

Post a Comment

0 Comments