Ticker

6/recent/ticker-posts

Christian Eriksen Ajiunga na United kwa Mkataba wa Kudumu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Christian Eriksen Ajiunga na United kwa Mkataba wa Kudumu 


Kiungo wa timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen amekubali kujiunga na klabu ya Manchester United baada ya kukamilika kwa mkataba wake wa miezi sita na klabu ya Brentford mwezi Uliopita. 

Usajili huo ungali kukamilika lakini kiungo huyo mbunifu anariporiwa kuridhia mkataba wa miaka mitatu na kuwa sehemu ya ukarabati unaotekelezwa na kocha mpya Erik ten Hag ndani ya Old Trafford. 

Klabu yake ya zamani Tottenham ilionyesha nia ya kumsajili lakini kocha Antonio Conte alipoelekeza nguvu zaidi kwa wachezaji wengine, United ikasalia na nafasi kubwa zaidi ya kumnasa Eriksen. 

Usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 utampiga jeki ten Hag ambaye kwa sasa anakabiliwa na tatizo la mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo kuweka wazi nia yake ya kuondoka klabuni hapo. 

Ronaldo hakuhudhuria siku ya kwanza ya mazoezi mnamo Jumatatu akitaja matatizo ya kifamilia kama sababu ya kukosekana kwake. United wamekubali maelezo yake lakini wamedinda kuw anyota huyo si wa kupigwa mnada na anatarajiwa kukamilisha miezi 12 iliyosalia katika mkataba wake. 

United imeipa kipaumbele zaidi idara ya kati, ten Hag anakaribia kumnasa Frenkie De Jong kutoka Barcelona lakini viungo wakabaji pia wanawindwa na miamba hao wa Old Trafford.

Beki wa kushoto wa Feyenoord Tyrell Malacia aliratibiwa kukamilisha vipimo vyake vya afya ili kuwa sajili wa kwanza wa ten Hag jijini Manchester huku pia United wakiwa wamewasilisha ofa ya kumtwaa beki wa kati wa Ajax Lisandro Martinez.

Post a Comment

0 Comments