Ticker

6/recent/ticker-posts

Kagere, Lwanga, Mhilu Waondoka Simba

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Kagere, Lwanga Na Mhilu Waondoka Simba, rasmi sasa msimu ujao wa mashindano ya ndani na yale ya kimataifa, Simba haitakuwa na washambuliaji wake wawili, Meddie Kagere na Yusuph Mhilu pamoja na kiungo mkabaji kutoka Uganda, Taddeo Lwanga baada ya mabosi wao kuwaaga rasmi.

Habari kutoka ndani ya Simba na kuthibitishwa na mmoja wa watu wa karibu wa Kagere ni wachezaji hao hawatakuwa sehemu ya kikosi, baada ya juzi kuitwa na uongozi na kuelezwa wazi, sambamba na kuagwa na hawatakuwa kwenye kikosi kuitakachoenda Misri kujiandaa kwa msimu mpya.

“Lwanga licha ya kuwa na mkataba, lakini ameelezwa atafute timu ili akatumike kwa mkopo sawa na Mhilu, lakini Kagere ndio hivyo ameshamaliza mkataba hivyo ana uhuru wa kutua kokote,” kilisema chanzo hicho.

Wachezaji hao wanaungana na Bernard Morrison, Pascal Wawa na Rally Bwalya walioagwa rasmi kuondolewa Simba, ili kupisha majembe mapya akiwamo Mzambia Moses Phiri, Augustine Okrah kutoka Ghana na Mnigeria Victor Akpan aliyekuwa Coastal Union.

Pia yumo Cesar Manzoki aliyekuwa Vipers ya Uganda sambamba na wazawa, Nassor Kapama, huku George Mpole ikielezwa tayari ana mkataba mkononi ila bado hajasaini kuvaa uzi mweupe na mwekundu kwa msimu ujao kutoka Geita Gold aliyopanda nayo msimu huu.

Soma Pia | Sopu Atua Azam FC

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez aliliambia Mwanaspoti mapema, uongozi wao ukishirikiana na benchi wanakitengeneza upya kikosi chao baada ya msimu huu kuwa mbaya kwa kupoteza mataji matatu iliyokuwa ikiyashikilia ikiwamo la Ligi, Ngao ya Jamii na ASFC, huku iking’olewa Ligi ya Mapingwa Afrika japo ilifika robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Naye kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola amesema wanahitaji kujipanga haswa ili kuhimili ushindani wa Ligi Kuu msimu ujao baada ya kupoteza makombe matatu msimu huu.

“Tumeteleza cha msingi ni kuangalia tulipoangukia na kuendelea na safari, tumepoteza makombe yote sio jambo dogo lakini ndio mpira,” alisema Matola na kuongeza kuwa wanahitaji kujipanga kuhakikisha wanarejesha heshima na mataji ndani ya msimu ujao.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi

Post a Comment

0 Comments