Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea: Hatuna Haja Tena Na Ronaldo

CHELSEA wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili fowadi mahiri wa Manchester United, Cristiano Ronaldo.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 37 aliwahi kutaka Man-United wamwachilie ajiunge na kikosi kipya muhula huu, tukio lililomfanya kivutio miongoni mwa klabu nyingi ikiwemo Chelsea.


Hata hivyo, kocha Thomas Tuchel amesema kubwa zaidi katika maazimio ya sasa ya Chelsea ni kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya mshambuliaji Raheem Sterling kuagana na Manchester City na kutua ugani Stamford Bridge.

Licha ya Ronaldo kutaka kuondoka ugani Old Trafford, kocha Erik ten Hag amesema sogora huyo wa zamani wa Real Madrid na Juventus angali katika mipango yake ya baadaye kambini mwa Man-United.

Ronaldo bado hajaungana na wenzake wa Man-United nchini Australia wanakopiga kambi ya mazoezi kwa ajili ya kampeni za msimu mpya wa 2022-23.

Chelsea wanahisi kwamba Sterling atawatambisha katika safu yao ya mbele zaidi ya alivyofanya Romelu Lukaku aliyesajiliwa na Inter Milan kwa mkopo.

Kwa mujibu wa Tuchel, Chelsea kwa sasa wanatarajiwa kusajili beki Kalidou Koulibaly kwa mkataba wa miaka minne kutoka Napoli huku wakihusishwa pia na uwezekano wa kujinasia maarifa ya Nathan Ake kutoka Man-City na Presnel Kimpembe wa Paris Saint-Germain (PSG).

Kimpembe ambaye ni raia wa Ufaransa, aliwahi kunolewa na Tuchel kambini mwa PSG kati ya 2018 na 2020.

Post a Comment

0 Comments