Ticker

6/recent/ticker-posts

Panga La Simba La Mkosa Gadiel Michael

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Panga La Simba La Mkosa Gadiel Michael

Simba ilikuwa na mipango ya kumtema Gadiel Michael ili imvute, beki wa kushoto wa Polisi Tanzania, Yahya Mbegu, lakini dili hilo limekufa, Wameamua kumbakisha kikosini.

Gadiel alikuwa na dili la kujiunga na Singida Big Stars ila mpango huo umeonekana kuwa mgumu kwa sababu iliyoelezwa timu hiyo itamchukua, beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustafa.

Baada ya dili hilo kuwa gumu Simba imekubali kuendelea kubaki na Gadiel kama mbadala wa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye ndio chaguo la kwanza kwa makocha wengi waliyopita kwenye kikosi hicho.

Kushindikana kwa Gadiel kwenda Singida maana yake dili la Mbegu lilikufa na kumfanya mlinzi huyo wa kushoto mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kufanya maamuzi mengine.

Taarifa za uhakika zinadai Mbegu baada ya dili la Simba kushindikana amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Geita Gold ambayo msimu ujao itacheza mashindano ya kimataifa.

Alipoulizwa Mbegu alisema kuendelea kubaki Polisi msimu ujao ni asilimia ndogo kutokana mkataba wake umefikia ukingoni na kuna maamuzi mengine ameyafanya tayari. “Kuna timu nyingine nitakwenda msimu ujao na wao ndio wanatakiwa kuwa wa kwanza kuweka wazi usajili wangu siyo mimi,” alisema Mbegu.

Usajili huo wa Mbegu Geita utaifanya timu hiyo kuwa na mabeki watatu wa kushoto, Adeyun Saleh na Amosi Charles. Wakati huo huo Geita imemnasa kiraka, Haruna Shamte kutokea Namungo.

Post a Comment

0 Comments