Ticker

6/recent/ticker-posts

Chelsea wakamilisha usajili wa Kalidou Koulibaly kutoka Napoli

Chelsea wamekamilisha usajili wa Kalidou Koulibaly kutoka Napoli kwa euro milioni 40m, huku beki huyo wa kati wa Senegal akisaini mkataba wa miaka minne Stamford Bridge.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa katika safu ya ulinzi ya ya Chelsea kufuatia kuondoka kwa Antonio Rudiger na Andreas Christensen baada ya kumalizika kwa mikataba yao.


Chelsea ilimgeukia Koulibaly wa Napoli baada ya mlengwa namba moja aliyepewa kipaumbele Matthijs de Ligt kushindwa kumpata. Juventus pia walimuhitaji sana Koulibaly achukue nafasi ya De Ligt anayekwenda Bayern Munich, lakini Napoli hawakuwa tayari kufanya biashara na wapinzani wao wa Serie A.

Hilo liliwapa Chelsea faida, na The Blues wameharakisha kukamilisha dili la €40m (£34m) kwa ajili ya beki huyo, ambaye amesaini mkataba utakaodumu hadi 2026.

Baada ya kufaulu vipimo vya afya huko London, Koulibaly amesafiri kuelekea Los Vegas kuungana na wachezaji wenzake kwenye ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya na ametambulishwa kama mchezaji wa Chelsea leo Jumamosi.

"Nina furaha sana kuwa hapa na timu hii ya Chelsea," Koulibaly aliambia tovuti ya Chelsea. “Ni timu kubwa duniani na ndoto yangu ilikuwa ni kucheza Ligi Kuu siku zote, Mara ya kwanza Chelsea walinihitaji mwaka 2016 lakini hawakufanikiwa, safari hii walipokuja kwangu nikawakubalia kwa sababu walinihitaji kuja kucheza Ligi Kuu.

"Nilipozungumza na marafiki zangu Edou [Edouard Mendy] na Jorginho walifanya uchaguzi wangu kuwa rahisi, hivyo nina furaha sana kuwa nanyi leo.'Nataka kuwashukuru mashabiki kwa sababu niliwaona wengi London na kwenye ndege kila mtu alifurahi  mimi kuwa hapa. Kwa hivyo nataka kuwashukuru na natumai msimu utakuwa mzuri sana na tutawapa wakati mzuri mashabiki zetu."

Mwenyekiti Todd Boehly aliongeza: "Kalidou Koulibaly ni mmoja wa mabeki mahiri na hodari duniani na tunafuraha kumkaribisha Chelsea."

Koulibaly alikuwa ameingia mwaka wa mwisho wa kwenye mkataba wake na Napoli baada ya kujiunga na klabu hiyo mwaka 2014. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal amekuwa akihusishwa na kuhama mara kadhaa huko nyuma, na inaonekana hatimaye ameamua kuwa ni wakati muafaka wa yeye Kuhama.

Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel anataka kuongeza mabeki wengine wawili wa kati kwenye kikosi chake msimu huu wa majira ya joto, huku mustakabali wa nahodha Cesar Azpilicueta ukiwa haujulikani. 

Post a Comment

0 Comments