Ticker

6/recent/ticker-posts

MANZOKI ATUA SIMBA, Vipers wamuwekea ngumu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MSHAMBULIAJI kutoka Vipers ya Uganda, Cesar Lobi Manzoki Juzi Ijumaa Alitua Dar es Salaam akitokea mapumzikoni kwao DR Congo baada ya kumaliza msimu akiwa kwenye mafanikio makubwa binafsi na timu kiujumla, huku kubwa ikiwa ni kushughulikia dili lake la kutua Msimbazi.

Hii ni mara ya pili kwa mshambuliaji huyo kutua nchini kimya kimya, kwani awali alitua na kusainishwa mkataba wa miaka miwili na Simba na safari hii amekuja ili kupigwa tafu juu ya kupata barua ya kuruhusiwa kuondoka kutoka Vipers ambao wameamua kuweka ngumu kwa madai bado wana mkataba naye, japo mwenyewe anasisitiza umeisha mwisho wa msimu huu.

Chanzo makini kutoka Uganda kilieleza Manzoki alisaini mkataba wa miaka miwili uliomalizika mwisho wa msimu huu, japo mabosi wa Vipers wameamua kukomaa naye na kumfanya ashindwe kuungana na wenzake Misri, licha ya jina lake kuwepo katika orodha ya watu 48.

“Manzoki ni mchezaji huru kwani mkataba wake wa miaka miwili amemaliza ila bahati mbaya nakala ya mkataba wake aliiweka kwenye simu ambayo ilipotea, hivyo hana ushahidi na hapo Vipers wamemchomekea mwingine wa miaka miwili,” kilisema chanzo makini kutoka Uganda.

Taarifa nyingine kutoka ndani ya Simba zinasema baada ya klabu kupambana kwa siku tatu ili kupata kibali cha kuruhusiwa kumtumia Manzoki, iliamua kumleta nchini ili washughulikie kwa kupitia wanasheria ili kupata kibali kutoka FUFA (shirikisho la soka la Uganda) na Vipers.

Manzoki, alipotafutwa alisema kwa ufupi; “Tusubiri kuna mambo ya kimsingi yanawekwa sawa, yakimalizika hayo itafahamika timu nitakayoitumikia msimu ujao, kwa sasa niache tu kwanza.”

Post a Comment

0 Comments