Ticker

6/recent/ticker-posts

Mukoko atua Dar, Azungumzia Usajili Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

KIUNGO wa zamani wa Yanga aliyetimkia TP Mazembe, Mukoko Tonombe yupo jijini Dar es Salaam na jana amevunja ukimya kwa kuelezea usajili uliofanywa na Yanga msimu huu utawabeba sana kwenye michuano ya kimataifa.

Mukoko alisema mastaa watano wa kigeni walioongezwa kikosini ni majembe ya maana akiwatolea mfano Bernard Morrison, Stephen Aziz Ki na Joyce Lomalisa aliodai wakiungana na nyota wengine waliosalia kikosini watawasumbua sana wapinzani kuliko msimu uliomalizaka hivi karibuni.


Yanga imesajili nyota watano tu na wote ni wa kigeni ambao mbali na Aziz KI, Lomalisa na Morrison, wengine ni Lazarous Kambole kutoka Zambia na Mrundi aliyekuwa akikipiga Ulaya, Gael Bigirimana. Sasa Mukoko aliliambia Mwanaspoti kuwa, uwezo wa mastaa hao kwa jinsi alivyowafuatilia kwa ukaribu na uzoefu wao kimataifa ni moja ya chachu ya mafanikio kwa Yanga ambayo haina cha kupoteza kwenye ligi ya ndani.

“Lomalisa ni beki mzuri anajua nini anakifanya akiwa uwanjani sitaki kumuelezea sana kwasababu tayari amefanya makubwa mengi na ninaamini atafanya kazi nzuri, KI, Bigirimana, Morrison na Kambole pia watakuwa na mchango zaidi kutokana na uzoefu wao,” alisema Mukoko na kuongeza;

“Yanga mbali na ujio wa mastaa hao ilikuwa tayari imekamilika na imeonyesha hilo kwenye mataji mawili makubwa ya ndani iliyotwaa bila ya kupoteza mchezo hata mmoja, hivyo ongezeko la mastaa hao ni chachu ya ushindani wa namba kulingana na ubora wa mtu na mtu.”

Mukoko alisema Yanga haijasajili mastaa wengi kwani tayari ina kikosi ambacho kimeweza kukaa pamoja msimu mmoja na kupata mafanikio makubwa hivyo anatarajia kuona walioingia katika dirisha hili la usajili wakiongeza nguvu na kuingia sambamba kikosini kutokana na uzoefu wa ligi ya Afrika huku akimtaja Morrison kuwa hakuna anachotakiwa kufundishwa.

“Misimu minne mfululizo walikuwa na utaratibu wa kuvunja timu na kuanza upya kitu ambacho kiliwanyima mataji, lakini msimu ulioisha walijipanga na kufanya vizuri kitu kilichozaa matunda,” alisema.

Post a Comment

0 Comments