Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi wiki tatu zinanitosha yanga

Kocha wa Yanga Nasreddine Nabi amewashusha presha mashabiki wao akisema bado muda upo na kwamba siku 21 tu zinamtosha kuunda timu na kufanya makubwa msimu ujao wa mashindano.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Tunisia aliko mapumzikoni, Nabi alisema suala la kambi yao lipo chini ya mabosi wa klabu hiyo, lakini akasema wala lisiwape presha mashabiki wao.

Nabi alisema kikosi chake kilichochukua mataji matatu msimu uliomalizika kinahitaji wiki tatu tu hadi kuiva na kuendeleza moto.

“Nafikiri suala la wapi tutaweka kambi hilo linafanyiwa kazi na viongozi naona kama watu wamekuwa na wasiwasi kutokana na kile kilitokea huko nyuma,” alisema Nabi na kuongeza;

“Tuna muda bado, wiki hii wachezaji wanamalizia mapumziko, sidhani kama tumechelewa sana labda watu wana kiu ya kutaka kujua wapi tutakwenda. Kama itaamuliwa wiki inayoanza kesho (leo) haitakuwa mbaya kwa kuwa hata wachezaji mapumziko yao yanaisha wiki hiyo, kama tukipata wiki tatu tutakuwa tumefanikiwa sana.”

Nabi aliyechukua tuzo ya Kocha Bora alisema kikosi chake hakihitaji mambo mengi sana kwa kuwa tayari wakati huu wana timu kamili na kitu muhimu ni kuwapata wachezaji wote ukiondoa waliopo kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars. “Wakati ule tulipata shida kwa kuwa timu yetu ilikuwa mpya kabisa ilihitaji muda mrefu.”

Post a Comment

0 Comments